Short note: This website is in Beta - we are currently building everything up but you can already find the apps to download and participate! Thank you and stay safe!

Jinsi ya kupima topetope

Topetope linaweza kupimwa kwa kutumia bomba la topetope (tazama picha hapa chini).

  ID 1685 turbidity tube

Bomba lina alama katika upande. Kiwango kikubwa kinaonyesha kuwa chembe nyingi zaidi huyeyushwa ndani ya maji na kwamba maji siyo meupe sana. Kwa upande wa ubora wa maji, kiwango cha chini ni bora zaidi.

Ili kupima topetope, hatua kadhaa zinahitajika:

Kwanza jaza maji kwenye jagi lililoshikiliwa na mnyororo kutoka mtoni. Jaribu kuchukua majiya juu ya uso wa mto na si kutoka kchin ya mto.

Kisha mimina maji kidogo kwenye bomba la topetope hadi ifikie alama ya kwanza (tazama mfano wa picha hapa chini).

ID 1685 first mark

Sasa angalia kwenye bomba la topetope kutoka juu. Je, unaweza kuona duara la kijani kibichi chini ya bomba?

ID 1685 green circle

 -Ikiwa huwezi kuona mduara wa kijani tena, soma thamani katika alama ya chini kabisa kwenye bomba na uweke thamani hiyo katika sehemu inayofaa katika programu ya HydroCrowd. Ikiwa mduara wa kijani bado unaonekana, jaza bomba hadi alama inayofuata. Rudia mchakato hadi ambapo hutaweza kuona mduara wa kijani tena.

ID 1685 no pattern

Ingiza thamani hiyo katika programu ambapo mduara haukuonekana tena.