Short note: This website is in Beta - we are currently building everything up but you can already find the apps to download and participate! Thank you and stay safe!

Jinsi ya kupima mvua

Mvua katika eneo fulani hupimwa kwa kipima mvua. Kwenye kituo, kipimo cha mvua kimewekwa upande wa kulia wa ubao wa taarifa (angalia mfano hapa chini).

  ID 1671 info board

Mvua hupimwa kwa milimita (mm). Alama zilizo kando ya kipimo cha mvua zinaonyesha ni kiasi gani cha mvua ilinyesha tangu mara ya mwisho kipima mvua kilipomwagwa. Kiwango kinagawanywa katika vipindi vya 1 mm (alama fupi) na 5 mm (alama ndefu). Kuangalia kiasi cha maji katika kipimo cha mvua. Simama mwenyewe, ili macho yako yawe kwenye urefu sawa na kiwango cha maji kwenye kipimo cha mvua (tazama mfano hapa chini).

ID 1671 rain gauge example

Alama iliyo karibu zaidi na kiwango cha maji katika kipimo cha mvua ni kiasi cha mvua. Katika mfano hapo juu mvua ni 10 mm. Baada ya kuwasilisha taarifa ya kipimo cha mvua, usisahau kumwaga maji katika kipimo cha mvua kwa kukigeuza juu chini na baadaye kukirudisha juu huku mdomo(inlet) ikielekea angani (kama ilivyo kwenye picha ya kwanza).